Kuitambulisha Shule ya Kitkit

Shule ya Kitkit ni zana ya kipekee ya elimu iliyojengwa ili kuwafundisha wajifunzaji wote wa awali kusoma, kuandika na hisabati. Imetajwa kama moja ya washindani bora katika shindalo la Ujifunzaji wa Kimataifa la XPRIZE.

Sisi ni nani

Enuma ni kampuni inayoongoza katika kutoa zana za kujifunzia za kidijitali kwa elimu ya awali ambazo zinaweza kutumiwa na watoto wote. Imeanzishwa mwaka 2012 ikiwa na dira ya kuwawezesha watoto wenye mahitaji maalumu kujifunza wakiwa peke yao, Enuma imefanya kazi kuweka viwango vipya kwa ajili ya uzoefu wa mtumiaji na muundo unaoweza kutumika kwa urahisi kwa mjifunzaji yeyote.