BidhaaShule ya Kitkit ni suluhisho kamili la elimu ya awali iliyotengenezwa kwa ajili ya watoto WOTE.

Tulitengeneza Shule ya Kitkit ili kutoa fursa ya kujifunza yenye ubora wa hali ya juu kwa watoto wenye uhitaji mkubwa dunia nzima. Jina hili limetokana na neno la Kithai "kufikiri", Shule ya Kitkit ni programu ya kompyuta ya kwenye tableti yenye mtaala wenye maarifa mengi unaowavusha watoto wenye umri wa awali katika elimu ya awali. Umeandaliwa ili kuwapatia watoto misingi na mazoezi yanayohitajika kujenga ujuzi wa msingi katika kujua kusoma na kuandika bila kujali kuwa na uwezo wa kwenda shuleni au kutumia nyenzo kama hizo. Shule ya Kitkit huweka pamoja desturi bora zaidi za kimataifa katika elimu ya kujua kusoma na kuandika na hisabati pamoja na kanuni za Utengenezaji wa Zana za Kujifunzia za Kimataifa ili kumsaidia kila mtoto kufanikiwa kama mjifunzaji anayejitegemea. Usanifu wake wa kujifunzia ambao unaendana na mazingira unatumika pamoja na picha za mazingira ya asili ambazo zinavuka mipaka ya kiutamaduni na kuwaunganisha wanafunzi wenye utamaduni tofautitofauti dunia nzima kuwa na matokeo mazuri ya kielimu.

Shule ya Kitkit hujumuisha michezo (magemu), vitabu, video na maswali ambayo huwasaidia watoto kufanyia mazoezi kusoma, kuandika, na kuhesabu na kufanya maswali ya hisabati. Programu hii ya kompyuta pia hujumuisha maktaba ambayo watoto wanaweza kuperuzi kwa uhuru, vilevile zana ambazo huhamasisha ubunifu ikiwa ni pamoja na ngoma, marimba na vifaa vya kuchorea vya kidijitali.

Jaribio la Ufaafu lililofanyika Afrika

Timu ya Shule ya Kitkit ilifanya majaribio matatu ya uwandani mwaka 2016. Majaribio haya ya uwandani yalijumuisha utafiti kwa njia ya kutazama kila siku, majaribio ya mahojiano ya kabla na baada ya jaribio kwa wanafunzi wa Darasa la 2, na jaribio la kidijitali la kabla na baada ya jaribio kwa washiriki wote. Majaribio yetu ya mahojiano yalitoa taarifa muhimu kuhusu kiwango cha mafanikio ndani ya maeneo ya kijijini na miji midogo Tanzania, pamoja na wanafunzi katika shule mbili tulizofanya majaribio zilipata alama za juu kwa wastani kuliko Utafiti wa Awali wa Taifa wa mwaka 2014 ulivyopendekeza. Hata hivyo, matokeo yetu hayakuchana na Utafiti wa Awali wa Taifa wa mwaka 2014 kwamba alama za watoto katika kusoma ufahamu na kufanya hesabu ngumu zaidi zilikuwa chini kabisa. Hivyo, wakati inaonekana dhana za awali (kama vile utambuzi wa namba, herufi na silabi) ni dhana za kukumbuka na ambazo ni rahisi kwa watoto, wanaweza kuhitaji usaidizi zaidi katika mazoezi ya dhana ngumu zaidi. Huku tukizingatia taarifa hizi akilini, tulifanya kuwa ni lengo letu kuhakikisha kuwa Shule ya Kitkit hutoa njia kadhaa ili waweze kufikiri kidhahania mapema katika mtaala. Kufanya hivi huhakikisha kwamba wanafunzi wanaanza kujenga msingi wa fikra dhahania kuanzia mwanzo, hivyo kuwafanya watumie fikra tunduizi na kutatua matatizo katika dhana changamani na mazoezi changamani zaidi pale yanapotokea. Inapofundisha kujumlisha na kutoa, Shule ya Kitkt hutoa si tu namba, lakini pia vitu katika ulimwengu halisi ili kuongeza uhusiano baina ya namba dhahania na uelewa wa mazingira ambamo mtoto anaishi.

Uchunguzi Kifani: Usanifu wa Shule ya Kitkit kwa watoto WOTE

Baada ya siku chache za uchunguzi wao wa programu katika moja ya shule za Utafiti Wetu wa uwandani, walimu walipendekeza kwamba tumjumuishe mwanafunzi mmoja wa Darasa la 3 mwenye dalili za ugonjwa wa akili. Mwanafunzi alishindwa kuhudhuria shuleni kwa miaka kadhaa, lakini aliruhusiwa kuendelea na madarasa bila kujali alama ndogo anazopata katika masomo. Familia ya mwanafunzi na walimu hawakuwa na matumaini ya juu au matarajio ya mafanikio, lakini badala yake waliona shule kama sehemu ya kupitisha muda kwake. Hata hivyo, baada ya kuwa amejumuishwa katika utafiti wa uwandani, walimu walishangazwa sana kuona furaha ya mtoto na maendeleo makubwa alipokuwa akichezea kifaa cha Shule ya Kitkit. Mtoto huyu hakuwa na uzoefu wa kutumia tableti hapo kabla, lakini aliweza kujua na kucheza michezo (magemu) kadhaa bila kuelekezwa. Walimu waligundua kwamba mchezo huu uliwezesha umakini wa mtoto huku ukitoa maudhui muhimu ya elimu. Na matokeo yake, walimu na familia ya mwanafunzi huyo waligundua kwamba kuna umuhimu mkubwa wa kujifunza kwa kutumia tableti kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

Majaribio yetu ya uwandani yalitoa mrejesho mzuri sana kutoka kwa wakuu wa shule na walimu. Mkuu wa shule wa shule ya msingi alitoa maoni kwamba Shule ya Kitikit ilifanya kujifunza kwa wanafunzi kuwa rahisi, kutokana na mazingira jumuishi na rafiki kwa mtoto imefanya iwe na ufanisi zaidi kuliko mtindo wa ufundishaji unapatikana katika madarasa mengi shuleni, na alishukuru sana kwa fursa ya kupunguza muda wa kutumia ubao kwa wanafunzi wake. Mwalimu mwingine aliona jinsi ambavyo mchezo huu ulikuwa wenye manufaa kwa wanafunzi wanaojifunza taratibu na wengine ambao wangeweza kunufaika na mazoezi mengi. Pia mwalimu mwingine alizungumza juu ya matokeo ambayo mchezo (gemu) huu unayo kwa shughuli ya wanafunzi pamoja na walimu: inahamasisha kufikiri kwa kina kuhusu elimu, huwahamasisha wanafunzi kuwa wabunifu zaidi katika kufikiri kwao.