Sisi ni nani

Shule ya Kitkit ilitengenezwa na timu maalumu kutoka Enuma ambayo ina uzoefu wa miongo kadhaa katika elimu, kutengeneza michezo ya kompyuta (magemu), uhandisi, usanifu, na maendeleo ya kimataifa.

Kuhusu Enuma na Shule ya Kitkit

Enuma ni kampuni inayoongoza katika kutoa zana za kujifunzia za kidijitali kwa elimu ya awali. Programu za kompyuta za kampuni zimetengenezwa ili kuwasaidia watoto wote kukuza uwezo wao wa awali katika kujua kusoma na kuandika na kuhesabu. Ilianzishwa mwaka 2012 na wataalamu wa kutengeneza michezo ya kompyuta ambao ni mume na mke wakiwa na dira ya kuwawezesha watoto wenye mahitaji maalumu kuwa wajifunzaji huru, Enuma ilitoa bidhaa yake inayoongoza kupata tuzo nyingi, Todo Math, mwaka 2014. Todo Math hutumia uzoefu mzuri wa mtumiaji na vipengele imara katika kuitumia ili kuwasadia wanafunzi wanaohangaika kujifunza kusonga mbele, na programu hii inaendelea kuwa moja ya programu za hisabati zinazofanikwa sana kwenye Apple App Store, ikiwa imepakuliwa mara milioni 3 dunia nzima.

Tuzo za Enuma na Utambuzi wa Todo Math

  • 2016 Google Play Programu Bora Zaidi ya Mwaka Korea, Familia
  • 2016 Tuzo za SIIA CODiE Mshindani Bora katika Zana Bora Kabisa ya Elimu ya Awali na Programu Bora Zaidi ya Elimu kwa Simu za Mkononi
  • Mshindi wa Tuzo ya Dhahabu ya Chaguo la Wazazi mwaka 2015
  • Mshindi wa Tuzo ya Ubunifu Bora Zaidi katika Mkutano wa Launch Education & Kids, 2013
  • Imepewa Nyota Tano za Ubora katika Common Sense Media

Timu ya Enuma sasa imetengeneza Shule ya Kitkit, zana yenya maarifa zaidi ya elimu ya awali ili kushughulikia tatizo la watoto milioni 250 duniani kote ambao hawajui kusoma wala kuandika. Imetengenezwa na timu ileile ya wataalamu waliojitoa, Shule ya Kitkit ni matokeo yanayoonekana ya malengo ya msingi ya Enuma ya kutoa zana za kujifunzia zenye ubora wa kimataifa kwa kila mtoto mwenye uhitaji. Timu hii imekuwa ikifanya kazi bila kuchoka kwa miaka kadhaa, ikifanya kazi kwa karibu na walimu wa hisabati, wataalamu wa elimu na walimu wanaofundisha darasani. Pia tumeendelea kuijenga timu yetu ya uhandisi na bishara. Sasa tunauona uwezo wetu kuwa:

Kweli ni zana iliyomlenga mtumiaji.

Timu ya Shule ya Kitkit huamini kwamba uhuru na ushirikishwaji ni sababu muhimu sana katika kutengeneza matokeo ya elimu yenye mafanikio mazuri kwa watoto. Kwa kujumuisha michezo ya kompyuta yenye ubora wa hali ya juu na utafiti katika vitendo kwenye elimu ya awali, sayansi ya akili na nadharia ya ujifunzaji, Shule ya Kitkit imekuwa ikishughulika na kuwaongoza watoto kujifunza peke yao bila kusimamiwa na mtu mzima.

Ubora wa kiufundi.

Pamoja na ubora wake wa juu katika matumizi ya mtumiaji, timu hii imetumia usanifu wa hali ya juu na mfumo imara wa seva uliowekwa katika viwango vya tasnia ya michezo ya kompyuta ili kuifanya Shule ya Kitikit kuwafikia mamilioni ya watumiaji.

Kuongozwa na data.

Katika kutengeneza programu za kompyuta, timu yetu hutumia matokeo ya utafiti katika sayansi ya akili, elimu maalumu na desturi bora zaidi za kimataifa katika kujifunza na elimu. Timu hii pia kwa usalama inakusanya, kuchakata na kutafsiri kiwango kikubwa cha data za watumiaji ambazo si za siri kutoka katika programu zetu za kompyuta, ambazo tunatumia kuboresha matokeo ya kujifunza na ufaaji wa kutumika. Tulitumia mbinu ile ile ya utafiti katika kutengeneza Shule ya Kitkit, ikiwa ni pamoja na kufanya majaribio ya uwandani nchini Kenya na Tanzania kwa kusudi la kuelewa ufaaji wa kutumika na ufanisi wa programu hii.

Kujizatiti katika kuwasaidia watoto waliotengwa na jamii.

Lengo la msingi la Enuma limekuwa ni kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalumu au tofauti za kujifunza, watoto ambao hawana nyenzo na watoto ambao hawawezi kuingia katika mfumo wa elimu bora. Mafanikio ya programu zetu za biashara ambazo tayari zipo — ikiwa ni pamoja na Todo Math, Kid in Story Book Maker [Mtoto katika Kitengeneza Kitabu cha Hadithi] na Visual Schedule for Children with Autism [Jedwali la Kutazama kwa Watoto wenye Ulemavu wa Akili] —zimethibitisha kujizatiti kwetu kutengeneza bidhaa bora kabisa ili kuwahudumia watoto wote.

Timu ya Shule ya Kitkit (zamani Timu ya Shule ya Todo) iliingia katika shindano la Ujifunzaji wa Kimataifa XPRIZE kwa sababu ya imani yetu isiyoyumba kwamba watoto ambao wanaweza kunufaika zaidi na zana za elimu za kiteknolojia ni watoto ambao kujifunza hakuwi rahisi kulingana na mazingira ambayo yapo nje ya uwezo wao. Timu yetu imeundwa na watengenezaji wa michezo ya kompyuta wanaoipenda kazi yao, walimu, watafiti, wataalamu wa TEHAMA na wataalamu wa biashara ambao wanataka kufikia ndoto ya kuwawezesha mamilioni ya watoto dunia nzima kujifunza peke yao.

Ushirikiano

Mradi huu umewezekana kwa ushirikiano wa Shirika la Maendeleo la Korea (KOICA), na washirika wetu wengine wazuri kutoka Afrika Mashariki.